Like Us On Facebook

Sunday, February 23, 2014

CHOKY AIBUKA UKUMBINI NA GARI LA KUBEBEA WAGOINJWA, AFANYA BONGE LA SHOO DAR LIVE AKIPIGWA TAFU NA BANZA STONE, MUUMINI

UZINDUZI wa albamu ya Mtenda Akitendewa ya bendi ya Extra Bongo usiku wa jana umefana kwenye ukumbi wa Dar Live, maarufu kama Uwanja wa Taifa wa Burudani, Mbagala, Dar es Salaam. Kivutio zaidi kilikuwa kiongozi wa bendi ya Extra, ‘Kamarade’ Ally Choky aliyeingia ukumbini na gari la kukimbizia wagonjwa mahututi hospitali, maarufu kama Ambulance ukumbini. Ambulance hiyo ilisindikizwa na pikipiki zaidi ya 30 zile ambazo mjini tunaziita bodaboda, ambazo zilipofika mbele ya jukwaa zilifanya fujo za kutosha hadi mojawapo kudondoka na kumjerujhi dereva wake.
Wapinzani wa zamani; Ally Choky kushoto akiimba na Banza Stone jana Dar LIve
Ally Choky akishuka kwenye Ambulance
Ambulance ya Choky ilivyopokelewa ukumbini
Ajali; Boda boda hii ilikula mwereka na kujeruhi dereva wake
Choky aliibuka kwenye mlango wa Ambulance akiwa peke yake na kupanda jukwaani moja kwa moja kuanza kuimba. Kwa kiasi fulani ilikumbushia enzi zile za msisimko wa muziki wa dansi  nchini kwa kiwango cha juu gwiji huyo alipokuwa akiingia ukumbini na Farasi, TingaTinga na kadhakika na kusababisha mpinzani wake mkuu enzi hizo, Banza Stone ampige kijembe “Kwenye Starehe Kijiko kimeingiaje”. Lakini jana Banza hakuwa mpinzani wa Choky, bali alikuwa mmoja wa wanamuziki waliyeimba naye jukwaa moja pamoja na Prince Mwinjuma Muumini ‘Kocha wa Dunia’ na bendi ya Tanzania One Theatre (TOT) upande wa Taarab.  Choky alipagawisha mashabiki kwa nyimbo kadhaa zilizosindikizwa na sebene la nguvu lililokuwa linapikwa na wataalamu wa ala wakiongozwa na Ephraim Joshua katika gita la besi. Utamu zaidi katika shoo zilizovurumishwa na wanenguaji mahiri na wasiozeeka viuno wakiongozwa na Super Nyamwela na Maria Sharapova.
Choky na mnenguaji wake
Choky na Muumin Mwinjuma
Maboda boda yakiongoza msafara wa Choky
Wanenguaji wakifanya yao jukwaani
Bin Zubeiry anapendwa na wengi sehemu nyingi,hapa nikiwa na mshakj wa Global Publisher kitengo Mawasiliano, ambaye ni kati ya wanaoendesha tovuti ya Global
Viongozi wa makundi ya TMK Wanaume Halisi, King Kiboya kulia na TMK Wanaume Family Said Fela kushoto walikuwepo
Mashujaa Bendi wakifanya yao jukwaani
Khadija Kopa TOT kushoto akipagawisha mashabiki
Amini na Linah kushoto wakifanya yao jukwaani
Kabla ya Choky kupanda jukwaani, bendi ya TOT Taarab ikiongozwa na Malkia Khadija Omar Kopa na Abdul Misambano ‘Super Rocky’ ilikata utepe na baadaye wakapanda Mashujaa kabla ya wanamuziki wa Bongo Fleva Fleva Amin na Linah kutoka THT kuvamia jukwaa. Idadi ya watu waliohudhuria onyesho hilo haikuwa kubwa sana, lakini si haba kwa hadhi ya sasa ya Choky na wote waliomsindikiza viliendana na ukumbi ulipendeza kiasi chake.
-BIN ZUBEIRY
Blogger Tricks

“Maisha yangu ni ya Kula Kulala”…Mzee Gurumo

MWANAMUZIKI ambaye kwa sasa amestaafu kuimba kwa sasa, Muhiddin Maalim Gurumo(Mzee Gurumo) amesema kuwa, tangu atangaze kuacha rasmi shughuli za muziki maisha yake ya sasa ni kula kulala kwani hana shughuli yoyote anayofanya.

Maisha Yake kwa Sasa.

Akipiga stori na paparazi wetu alisema, maisha yake ya sasa ni kusubiri giza liingie na jua liwake mkono uende kinywani kwa kuwa hana biashara yoyote anayoiendesha ya kuweza kumpatia ridhiki, mara nyingi huwa anajipumzisha kwenye baa ya Amana akiifariji nafsi yake.
Mzee Gurumo
Mzee Gurumo akiwa amepozi Amana Bar.

“Makazi yangu makubwa mimi ni kwenye baa ya Amana hapa sinywi pombe wala sivuti bangi napoteza muda saa ya kula ikifika nakula ya kulala nalala sitaki kujichosha uzeeni, wapo wengi tu wanaonitunza kuhakikisha sipati tabu kifedha,”alisema Mzee Gurumo.
CREDIT: GPL

AFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA KUMNAJISI MTOTO !!

MKAZI wa mtaa wa Nsemulwa, Athuman Mussa (54) amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumnajisi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne mdomoni.

Hukumu.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Ntegwa baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka uliongozwa na Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Juni 26 mwaka jana saa 12:00 jioni nyumbani kwake katika mtaa wa Nsemulwa katika Mji wa Mpanda.

Kumnajisi Mtoto

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Ntengwa alieleza kuwa siku hiyo ya tukio mshitakiwa alimkuta mtoto huyo ambaye wazazi wake ni jirani zake akiwa anacheza na watoto wenzake karibu na nyumba yake akamwita na kuingia naye ndani akiahidi kumpatia zawadi ya pipi aina ya jojo.
Baada ya mtoto huyo kuingia ndani ya nyumba, Athumani alimvuta kwenye kochi sebuleni na kisha alimwingizia uume wake kwenye mdomo wa mtoto huyo hadi hapo alipomaliza haja yake kisha akamwamuru aondoke nyumbani kwake ndipo mtoto huyo alipotoka mbio na kurejea kwao akilia.
 Kumnajisi
Aliiambia mahakama baada ya mtoto huyo kufika nyumbani kwao mama yake alimuuliza kilichomfanya alie ndipo alitema mbegu za kiume ambazo zilikuwa mdomoni mwake na kisha alimwelezea mama yake kila kitu alichotendewa na mshitakiwa.
Baada ya mama kuelezwa unyama huo wa Kumnajisi mtoto wake, naye alianza kulia kwa nguvu na kusababisha majirani kufika nyumbani hapo ambapo walielezwa alichofanyiwa mtoto huyo ndipo majirani walikwenda nyumbani kwa mshitakiwa wakamkamata na kumfikisha kwenye kituo cha polisi Wilaya ya Mpanda Jijini DAR.
Source: Habari Leo

Wanataaluma wayakosoa matokeo ya kidato cha nne 2013.



Siku moja baada ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kutangaza matokeo ya kidato cha nne na kuonyesha ufaulu kuongezeka kwa asilimia 15, wadau wa elimu wamepinga matokeo hayo kwa madai kuwa ubora wa elimu haukuangaliwa. 
 
Hatua hiyo inatokana na mabadiliko ya viwango vipya vya alama za ufaulu yaliyofanyika Oktoba mwaka jana, baada ya Serikali kuweka alama za kufaulu zisizobadilika katika daraja A mpaka F iliyotambuliwa kama kufaulu kusioridhisha.
 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ali alisema licha ya kiwango cha ufaulu kuongezeka, hakuna ubora wa elimu uliozingatiwa. Dk Ali alisema kinachochangia hali hiyo ni kuwapo kwa mfumo wa elimu wa kibaguzi, unaosababisha ubora wa elimu unashuka, kwa kuwa badala ya kupimwa kwa ujuzi na maarifa hupimwa kwa madaraja.
 
Dk Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Duce), alisema tatizo lililopo ni mfumo mbaya wa ufundishaji, badala ya kuwekeza nguvu kukuza taaluma, nguvu nyingi zimewekezwa kupanga madaraja.
 
Alisema matokeo hayo ni mazuri kwa Serikali, kutokana na kuzongwa na matokeo mabaya ya mwaka jana, lakini kitaaluma siyo mazuri.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari